Hukumu ya mke wa Bilionea Msuya inasomwa muda huu
Hukumu iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, ya mjane wa bilionea wa madini, Bilionea Msuya, Miriam Steven inasomwa muda huu.
Miriam pamoja na mshtakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, wanakabiriwa na shtaka la mauaji ya kukusudia, wanadaiwa kumuua kwa kumchinja, Aneth Elisaria, mdogo wa marehemu bilionea Msuya.Hukumu hiyo inasomwa na Jaji Edwin Kakolako, ambayo ndiyo itaamua hatima yao kama wana hatia au lah. Kama watakutwa na hatia hukumu ni kunyongwa hadi kufa.
Watuhumiwa wamekuwa mahabusu kwa miaka nane na leo ndio hatima yake, je, nini kitatokea leo Mambo yatakuwaje? Nini itakuwa hukumu ya kesi hii? Mke wa Msuya na mwenzake watakutwa na hatia au lah?
Mjane wa Bilionea Msuya alikuwa anatetewa na Wakili Peter Kibatala.

Post a Comment