CHANGAMKIENI FURSA ZA SEKTA YA UTALII

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao wanayozalishwa nchini na usafirishaji. 

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua  Mkutano wa pili wa Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho "The Z Summit 2024" katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar tarehe: 21 Februari 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea  kujenga miundombinu ya ujenzi wa barabara mpya, kuboresha usambazaji wa umeme na  maji pamoja na  viwanja vya ndege.

Halikadhalika, Rais Dk Mwinyi amesema Sheria mpya ya uwekezaji  Zanzibar ya mwaka 2024 imeweka vivutio vingi ambavyo vinalinda uwekezaji na  kuwa vivutio  vya kodi Afrika Mashariki. 

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Pemba ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya baadae kwa kuanzishwa ukanda wa uwekezaji wa Pemba (PIZ)  ili kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.


No comments