Winga wa Morocco, Hakim Ziyech 30, anaweza kurejea Chelsea
Nottingham Forest imeanza mazungumzo na Paris St-Germain kuhusu kumsajili tena kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 37, ambaye alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo kwenye Uwanja wa City Ground. (Football Insider)
Newcastle United inamtaka mlinzi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 19 Mbrazil, Andrey Santos, ambaye usajili wake kwa mkopo huko Nottingham Forest unatarajiwa kusitishwa mwezi huu. (Football 365)
Winga wa Burnley, Manuel Benson, 26, yuko kwenye mazungumzo na Hull City baada ya vilabu hivyo kukubaliana kwa mdomo mkataba wa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Hull Daily Mail)
Fulham wameongeza mkataba wa mwaka mmoja kwa nahodha wa klabu na kiungo wa kati wa Scotland Tom Cairney, 32, baada ya kiwango chake cha hivi karibuni kuwa kizuri. (Sun)
Chelsea wameanza mchakato wa kumsajili beki wa Nice na Ufaransa, Jean-Clair Todibo, 24, ambaye pia anawindwa na Manchester United na Tottenham. (Teamtalk)
Chelsea wanamtaka mshindi wa Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17 wa Ujerumani, David Odogu na mlinzi wa Wolfsburg mwenye umri wa miaka 17, ambaye hajacheza katika ligi ya Bundesliga. Pia anawindwa na Leicester City. (Sun)
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela, 34, anaweza kurejea Real Sociedad kwa mkataba wa muda mfupi. Mchezaji huyo wa Mexico pia anawindwa na Cruz Azul baada ya mkataba wake na Los Angeles FC kumalizika. (AS Diario)

Post a Comment