Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 02.01.2024
Liverpool na Real Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 yuko huru kusaini klabu nyingine mwezi huu. (Le Parisian)
Paris St-Germain wanawania saini ya kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, kutoka Manchester City mwezi huu. (Telegraph)
Manchester United na Liverpool wanaongoza mlolongo wa vilabu vinavyomtaka kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, 28, mkataba wake na Bayern Munich utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (AS)
Liverpool na Tottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Wolves na Korea Kusini, 27, Hwang Hee-Chan. (Football Insider)
West Ham wamewasiliana na Tottenham kuhusu kumnunua beki wa Uingereza, Eric Dier, ambaye yuko nje ya uwanja tangu kuwasili Ange Postecoglou. (Football Transfers)
Manchester City ni miongoni mwa timu inayomfuatilia mlinzi Leny Yoro mwenye umri wa miaka 18, huku Lille ikitaka pauni milioni 78. (Manchester Evening News)
Winga wa Morocco, Hakim Ziyech 30, anaweza kurejea Chelsea mwezi huu kwani Galatasaray inapanga kusitisha uhamisho wake wa mkopo wa msimu mzima. (NTV Spor)
Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kati wa Genoa raia wa Denmark, Morten Frendrup, 22, lakini uhamisho wa mwezi Januari huenda usifanikiwe. (Liverpool Echo)

Post a Comment