Waziri Mkuu Majaliwa awataka viongozi NAM kuhudhuria matukio
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesisitiza Wakuu wa Nchi na Serikali Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) wahakikishe wanashiriki katika kila tukio la umoja huo pamoja na kuendeleza ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ameyasema hayo jana Ijumaa, Januari 19, 2024 wakati akihutubia katika Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali zisizofungam
ana na Upande wowote (NAM) ulioanza tarehe 15 - 20 Januari, 2024. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
“Tumezungumzia hali ya mabadiliko ya tabia nchi na namna tunavyopata athari kwenye maeneo yetu na umuhimu wa kuweka mkakati wa namna ya kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye maeneo yetu.”
Masuala mengine ambayo Majaliwa aliyawekea msisitizo katika mkutano huo ni pamoja na kutoa wito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa kuangalia ajenda za NAM na kuona namna ya kushirikiana na NAM katika kuzitekeleza.

Post a Comment