Serikali kujenga minara ya mawasiliano eneo lililoathirika na mafuriko Hanang
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) ametembelea na kuona sehemu zilizoathiriwa na maporomoko ya matope Wilayani Hanang, kukagua miundombinu ya Anuani za Makazi na Posta pamoja na kuongea na waandishi wa habari.
Waziri Nape amevishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya kuhabarisha umma kipindi chote ambacho Wilaya ya Hanang ilikumbwa na janga kubwa la maafa.
Waziri Nape Nnauye amesema Serikali imeandaa minara zaidi ya 30 ambayo itasaidia kupunguza changamoto ya mawasiliano katika kata ya Gendabi na maeneo mengine ya Mkoa wa Manyara.
Nimemshukuru Mhe Nape kwa kusudio lake la kuhakikisha mawasiliano ya simu kwenye maeneo ya vijijini katika Mkoa wa Manyara yanaimarishwa

Post a Comment