Bashe: Bei ya sukari kuimarika mwezi ujao
Waziri wa kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe amesema serikali imeruhusu kuingizwa kwa tani laki moja ya sukari toka nje kutokana na hali ya uzalishaji wa viwanda vya ndani kuathiriwa na mvua kubwa za elnino zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza jijini Dodoma leo, Bashe amesema sukari hiyo inatarajiwa kuanza kuingia nchini Jumatano ijayo.
Waziri Bashe amewaomba Watanzania kuwa hali hii ya bei ya Sukari itakayoendelea kuimarika itarejea katika utulivu katikati ya mwezi februari huku akiyataka makampuni kuhakikisha hayafichi sukari au kuruhusu kupaa kwa bei kwa gharama ya Mlaji.

Post a Comment