MHE. DOROTHY MBUNGE TEMEKE, MHE DOROTHY WAZIRI, WASHIRIKI CHAKULA NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WILAYA YA TEMEKE.
Mhe Dorothy George Kilave Mbunge wa Jimbo la Temeke ameungana na Mhe Dkt. Dorothy Gwajima Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, na Viongozi wengine ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata, Kushiriki Chakula na Watoto wanye Mahitaji Maalumu Katika Kituo cha "Human Dream " Kilichopo Toangoma Wilaya ya Temeke.
Katika Tukio hili la Chakula Cha Pamoja na Watu Wenye Mahitaji Maalumu, Mhe Dkt Gwajima Waziri, Dorothy Kilave Mb, Na Viongozi wengine wamebainisha kuwa Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan imepitisha Sera Mbalimbali katika kuyalea na kuyatunza Makundi Maalumu Katika Jamii, hivyo ni wajibu kwetu kuhakikisha Makundi Maalumu yanapata Mahitaji na Ustawi katika Jamii, Ndio Hitaji kubwa la Rais Dkt, Samia na Serikali yake.
Aidha, Dkt Gwajima, Waziri. Ametoa Pongezi kwa Mhe Dorothy Kilave, Mbunge Temeke kwa Namna anavyojitoa na Kuyathamini Makundi Maalumu Katika Jamii, maana hata katika Mwezi Disemba 2023, amepeleka Mahitaji na kushiriki Chakula na Watoto Wenye Mahitaji Maalumu Katika Vituo Mbalimbali Jimboni Temeke.
Mhe Dorothy George Kilave Kwa Maendeleo ya Jimbo la Temeke.

Post a Comment