Uwanja wa Uhuru Dar wafungiwa

Uwanja wa Uhuru wa jijini Dar es Salaam umefungiwa kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kubainika kutokidhi vigezo na masharti yanayoongoza michuano hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Afisa Habari, Cliford Ndimbo, Shirikisho la Soka Nchini TFF, limesema timu zote ambazo zinautumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani, zitapaswa kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya mechi zake.

No comments