Simba yaduwazwa Chamazi

Timu ya Simba ambayo bado inajitafuta kurudi kwenye ubora wake, jioni hii imejikuta ikiduwazwa ndani ya dimba la Chamazi baada ya kubanwa sare ya mabao 2-2 na KMC, zote za jijini Dar es Salaam.

KMC walikuwa wa kwanza kuingia kambani katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Junior, lakini Simba wakasawazisha kipindi cha pili kwa penati ya Ntibanzonkiza.

Dakika moja baadae wakapata bao la pili kupitia kwa Bareke. Wakati kila mmoja akiamini Simba wataondoka na pointi zote tatu, kwa mara nyingine Junior aliingia kambani baada ya mlinda mlango Ayoub Lankred kuutema mpira.

Licha ya kuambulia pointi moja, lakini matokeo hayo yamewaumiza mno mashabiki wao ambao bado hawaelewi kuna nini kwa timu yao.

No comments