Aziz Ki aendeleza shangwe Jagwani

Aziz Ki, raia wa Burkina Faso, ambaye ndiye mchezaji muhimu zaidi katika kikosi cha mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, jioni ya leo ameendeleza shangwe mitaa ya Jangwani na Twiga, baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Tabora United.

Katika mechi ngumu iliyopigwa usiku huu katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aziz, ambaye ni kinara wa wafungaji wa Ligi Kuu, alipiga bao na kufikisha mabao 10.

Ushindi huo, unaoifanya Yanga sasa kuisogelea kwa karibu Azam iliyo kileleni ambayo hata hivyo, ina mochezo mitatu mbele, unawapa burudani ya kutosha mashabiki wake, wanaofadhiliwa na tajiri asiye na makeke, GSM.

Hii inakuja baada ya mahasimu wao wa miaka yote, Simba, kutoka sare na wakusanya kodi wa Kinondoni KMC kwa mabao 2-2 pale Chamazi Complex.

No comments