Mchengerwa aelekeza Uteuzi wa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera kutenguliwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed O. Mchengerwa amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Adolf Ndunguru kutengua uteuzi wa Kaimu Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Dr. Issesanda Kaniki na kupangiwa kazi nyingine

Maelekezo hayo ni baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi kuhusu ukosefu wa huduma bora za Afya kwenye baadhi ya Vituo vya kutolea huduma pamoja na kauli zisizoridhisha kutoka kwa baadhi ya watoa huduma za Afya

Mnamo Novemba 27, 2023 Mwananchi alilalamikia Kituo cha Afya cha Zamzam katika Manispaa ya Bukoba akidai hakina huduma nzuri kwa Wajawazito, Wahudumu kutojali wenye uhitaji, kuwapuuzia na kuwajibu vibaya na baadhi ya Watumishi kutengeneza mazingira ya Rushwa ili kutoa huduma ya haraka kwa Wanufaika wa Bima ya NHIF


  • Thanks
 Reactions

No comments