Mbwa aina ya XL kuuawa baada ya kumshambulia mmiliki alipokuwa akifanya ngono

 


Mbwa wa Kimarekani, XL bully amemshambulia mmiliki wake alipokuwa akifanya ngono, mahakama imeelezwa.

Mbwa huyo mwenye umri wa miaka miwili anayeitwa Hank alimuuma Scott Thurston, 32, nyumbani kwake huko Glanaman, Carmarthenshire, tarehe 2 Agosti.

Mahakama ya Llanelli ilielezwa kwamba mwenza wake Leanne Bell aliita polisi wafike Jones Terrace mapema asubuhi.

Amri ilitolewa kwamba mbwa huyo aangamizwe, hata hivyo, hilo halitafanyika kwa angalau siku 28 ikisubiri rufaa yoyote inayotolewa.

Picha za kamera za mwili zilizopigwa na maafisa ziliwaonesha wakiwasili kwenye eneo hilo, na Bw Thurston anasikika akijaribu kumziba mdomo mbwa huyo kwenye bustani.

Bi Bell alisikika akiwaambia maafisa hao wawili wa polisi: "Nina watoto wanne, nampenda mbwa, lakini siwezi kumruhusu kuwa karibu na watoto wangu."

Mahakama iliambiwa kwamba Bi Bell na Bw Thurston walikuwa wakizozana kabla ya kujamiiana, na mbwa huyo alimshambulia na kumng'ata Bw Thurston walipoanza kufanya ngono.

Bw Thurston aliumwa kwenye mkono wake wa kushoto na kidevuni, lakini alikataa kuchukuliwa na gari ya kubeba wagonjwa.

Mbwa hatimaye aliwekwa kwenye chumba cha chini. Polisi baadaye walimkamata mbwa huyo tarehe 19 Agosti, na amekuwa akiwekwa kwenye vibanda katika makao makuu ya Polisi ya Dyfed-Powys.

Kikosi hicho kilikuwa kikitafuta amri ya kuharibu chini ya Kifungu cha 2 cha Sheria ya Mbwa ya 1871, kwa misingi kwamba mbwa huyo alikuwa hatari.

Mahakimu walitoa amri ya uharibifu kwa msingi kwamba walikuwa na "maswala makubwa ya ulinzi" kuhusu mbwa huyo mwenye watoto wadogo wanne katika kaya hiyo. Walisema "haingeweza kurudishwa salama". Agizo la gharama ya £800 lilifanywa pia. Bw Thurston na mshirika wake Leanne Bell walikataa kutoa maoni yao walipokuwa wakitoka mahakamani.

No comments