Jamal Khashoggi: Mjane wake apata hifadhi ya kisiasa Marekani

 


Mjane wa mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, aliyeuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki amepewa hifadhi ya kisiasa nchini Marekani.

Jamal Khashoggi aliuawa mwaka 2018 na ujasusi wa Marekani unasema wanaamini Saudi Arabia ilihusika na mauaji hayo.

Mjane huyo, Hanan Elatar, alihofia usalama wake na alikwenda Marekani kuomba hifadhi Agosti 2020.

Hanan ameiambia BBC kuwa maisha yake yatakuwa hatarini ikiwa atarejea Misri au UAE.

BBC ilikagua hati zinazoonesha alipewa hifadhi ya kisiasa kwa muda usiojulikana Novemba 28.

Jamal Khashoggi aliyekuwa uhamishoni Marekani alikuwa akiandika makala zinazomkosoa mwanamfalme Mohammed Salman na serikali ya Saudi Arabia, aliuwawa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 2018.

No comments