Profesa Jay apokewa bungeni kwa shangwe

 


MSANII mkongwe wa Hip Hop ambaye pia alikuwa mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia Chadema, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, leo amewasili mjengoni mjini Dodoma na kupokewa kwa shangwe kubwa na wabunge.

Jay, ambaye aliishi katika Chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa changamoto ya Figo kwa zaidi ya siku 400, alifika bungeni kwa ajili ya kuitambulisha Taasisi yake ya Profesa Jay Foundation, ambayo itajihusisha na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Figo.

Aidha, wabunge wakiongozwa na Spika, walikubaliana kumchangia mwanamuziki huyo ambaye pia aliwaalika wabunge kuhudhuria uzinduzi  wa taasisi yake hiyo Novemba 24 mwaka huu, itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

No comments