Makumi ya watoto njiti hatarini kupoteza maisha Hospitali ya Al-Shifa Gaza
Makumi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wanaotibiwa kwa sasa katika hospitali ya Al-Shifa hawawezi kuhamishwa salama, shirika la misaada limesema.
Kufuatia jeshi la Israel kusisitiza kwamba limejitolea kusaidia kuhamisha watoto hao wachanga hadi "hospitali salama", Shirika la Msaada wa Matibabu kwa Wapalestina linasema kuwa harakati za kuwahamisha watoto wachanga walio wagonjwa mahututi ni "mchakato mgumu na wa kiufundi".
Katika taarifa yake siku ya Jumapili, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la misaada, Melanie Ward, alitilia shaka madai ya Israel na kusema "anatiwa wasiwasi sana na ripoti zisizo za kukosoaji za vyombo vya habari".
''Huku magari ya kubebea wagonjwa hayawezi kufika hospitalini - hasa wale walio na ujuzi na vifaa vinavyohitajika kuhamisha watoto hawa - na hakuna hospitali yenye uwezo wa kuwapokea, hakuna dalili ya jinsi hii inaweza kufanyika kwa usalama."
Ward anasema "chaguo pekee lililo salama" la kuokoa watoto wachanga ni kwa Israel "kusitisha mashambulizi yake na kuzingira Al Shifa, kuruhusu mafuta kufika hospitalini, na kuhakikisha kwamba wazazi waliobaki wa watoto hawa wanaweza kuunganishwa nao" .

Post a Comment