KICHWA CHA TRENI SGR CHAWASILI
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema kichwa kimoja cha reli ya kisasa kimewasili nchini kutoka Korea Kusini, tayari kwa zoezi la majaribio kwa safari za Dar es Salaam kwenda Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TRC, kichwa hicho chenye uwezo wa kuvuta mabehewa 14 ya abiria na kulisha umeme, ni miongoni mwa vichwa 17 vilivyoagizwa.
Aidha, shirika limesema ujenzi wa reli hiyo ya kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kimefikia asilimia 98 na majaribio hayo yanatarajiwa kufanywa mwezi mmoja ujao.

Post a Comment