Jeshi la Israel linasema wanajeshi 44 wa Israel wamefariki tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini huko Gaza
Jeshi la Israel limesema siku ya Jumatatu kuwa wanajeshi wengine wawili wamefariki wakati wa mapigano kaskazini mwa Gaza.
Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini imeongezeka hadi 44.
Jeshi la Israel limesema kuwa linaendelea na mashambulizi kwenye viunga vya kambi ya wakimbizi ya Al-Shati magharibi mwa Mji wa Gaza.

Post a Comment