HAMAS YADAIWA KUJENGA MIUNDOMBINU YA KIJESHI CHINI YA JENGO LA HOSPITALI
Mshauri mkuu wa Waziri Mkuu wa Israel Mark Regev, amedai kuwa Hamas ndio wa kulaumiwa kwa kugeuza hospitali ya Al-Shifa - kubwa zaidi huko Gaza - "kuwa eneo la vita".
Katika mazungumzo na BBC, alisema Hamas "imejenga kimakusudi" miundombinu ya kijeshi chini ya hospitali hiyo na "imewatumia watoto hao kukinga mashine zake za kijeshi".
Hamas na maafisa wa hospitali pia wamekataa mara kwa mara madai haya yanayohalalisha mashambulio ya Israeli karibu na hospitali za Ukanda huo. Regev alidai kuwa Israel haikujadili kulenga hospitali.
Alisema Hamas walitaka "picha zionyeshe shida" na hawakuwa tayari kukubali suluhisho la mafuta ili hospitali iendelee kufanya kazi.

Post a Comment