Rais Samia aweka shada kaburi la Dkt. Kaunda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa uhuru wa Zambia.

Rais Samia ameweka shada hilo ikiwa ni ishara ya kutoa heshima na kutambua walioongoza harakati za kuliltea uhuru Taifa hilo mwaka 1964

.Baada ya kuweka shada kwa mashujaa, Rais Samia pia ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda jijini Lusaka.

No comments