MWANAFUNZI WA SHERIA AITWA VITANI ISRAEL, AKUBALI KUPAMBANA NA HAMAS



Binti mwenye umri wa miaka 23, anayesomea sheria nchini Uingereza, Kinneret Hamburger ameitwa kujiunga na jeshi la Israel ambalo liko vitani na kundi la Hamas la Palestina. Jumla ya vijana 300, 000 wameitwa ili kwenda kuihami nchi yao na wote wamekubali kuingia Gaza.

Binti huyo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa klabu ya soka ya Manchester United, amekubali wito huo na yupo tayari kwa lolote, akisema yupo tayari kufa kwa ajili ya nchi yake, ubinadamu na nchi za Magharibi.

Luteni huyo wa Jeshi la Israel la IDF, amesema kikundi hcho cha kigaidi siyo tu ni adui wa nchi yake, bali kwa ulimwengu wote wa Magharibi.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa pili wa sheria alikuwa akiishi hotelini wakati wa likizo yake Oktoba akiwa na familia yake, aliposhtushwa na mashambulizi ya anga kutoka kwa Hamas. Wito wa kumtaka kambini ulimfikia siku moja tu kabla hajahamia kwenye jengo liingine. Aliendesha gari lake hadi kambini bila hata ya kuwa na begi lake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, mama yake Kinnenet, Maryon ambaye ana umri wa miaka 54 akiwa ni injinia katika kiwanda cha nguo, alikutana na baba yake Carl (56) wakiwa Chuo Kikuu cha Manchester.

Baadaye walitengena na kila mmoja akarejea nyumbani Israel kivyake, kabla ya kukutana na kuoana ambapo walifanikiwa kuzaa watoto wanne, wa kiume wa tatu na binti yao pekee, Kenneret,

Akijisikia fahari kulitumikia jeshi la Israel, IDF, Kinneret anasukumwa na morari ya kuitetea nchi yake ambayo anasema imezungukwa na viongozi wanaowafundisha watoto wa kizazi kijacho kuwa yeye na wayahudi wenzake wanapaswa kufa.

Amesema hakutakuwa na maswali wakati atakapofyatua risasi ya bunduki yake akisema hana chaguo kwa vile Hamas ndiyo wameanzisha vitsa.

Amedokeza kuwa ujio wa viongozi wa nchi za magharibi, akiwemo Joe Biden wa Marekani na Waziri Mkuu Rishi Sunak wa Uingereza, kuwa ni ushahidi wa wazi kwamba wameguswa wakiamini ugomvi huo unaweza kusambaa hadi nchi za magharibi.

FIGHTING FOR EVERYONE WHO VALUES LIFE: Kinneret insists she is not just fighting for her life and Israel, but for the whole of the western world


The law student said that visits from world leaders, including President Joe Biden and Rishi Sunak reinforce Israel's role in fighting for the West


No comments