Harry Styles atajwa tajiri kijana Uingereza akiwa na utajiri wa pauni milioni 175, mtoto wa David Beckham ana milioni 10

 






Harry Styles ametajwa kuwa mtu maarufu mwenye fedha nyingi miongoni mwa vijana walio na umri chini ya miaka 30, ikiwa ni mara ya pili mfululizo, akiwa na utajiri wa pauni za Uingereza milioni 175, sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 437.5.

Mtoto wa staa wa soka wa zamani England, David Beckham aitwaye Brooklyn Beckham akitajwa kuwa na utajiri wa pauni milioni 10, sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 25, zinazotokana na mapato kupitia matangazo ya kampuni mbalimbali, uanamitindo na ubalozi wa bidhaa kadha, katika umri wake wa miaka 24.

Harry, ambaye ni mwanamuziki, utajiri wake umeongezeka kutoka pauni milioni 150 mwaka jana, kufuatia kuingia mikataba mipya aliyoingia hivi karibuni ya kushiriki katika maonyesho ya mavazi na uanamitindo.

Broonklyn


No comments