MAKONDA USO KWA USO NA CHONGOLO
Uteuzi wa jana wa Katibu wa Itikadi, Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM Paul Makonda, unaenda kumkutanisha uso kwa uso na Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Daniel Chongolo.
Wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja, Makonda akiwa bosi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam huku Chongolo akihudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Makonda amekua nje ya ulingo wa siasa mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita, baada ya jaribio lake la kuwania ubunge kugonga mwamba baada ya kura zake kutokutosha katika kura za maoni jimboni Kigamboni.
Uteuzi wa Makonda kwa nafasi hiyo kubwa ndani ya chama umepokewa kwa hisia tofauti na wanachama, wapinzani na wananchi kwa ujumla.

Post a Comment