Ukraine: Wanajeshi ambao hawataondoka mstari wa mbele hadi vita viishe

 

Maisha kwenye mstari wa mbele wa vita vya Ukraine sio rahisi, BBC ilikwenda kushuhudia.

Akiwa amesimama katikati ya magofu ya majengo, Jimmy, afisa wa Ukraine - amefanya kazi kwa miaka mingi katika jeshi, alitafakari kuhusu maisha yake na kusema, "kwa ninavyoona mimi ni mwenye bahati."

Jimmy (jina la lakabu) anaongoza kikosi cha 24 kiitwacho Mechanized Brigade, kina historia ndefu, ni sehemu ya jeshi la kawaida la Ukraine, linalopigana na Warusi toka 2014. Tangu uvamizi wa Februari 2022, kikosi hicho kimeongezeka zaidi ya mara tatu kwa ukubwa.

Mwezi Agosti tulitumia wiki mbili, kwenye kituo cha zamani cha viwanda vya sigara upande wa mashariki tukiwa na kikosi cha 24, kinachopigana huko Donbas. Ni kikosi cha mstari wa mbele kati ya Bakhmut na Horlivka.

Kabla ya vita, Brigedi ya 24 ilikuwa na wanajeshi 2,000, wakigawika katika makundi matatu. Ingawa jeshi la Ukraine ni mara chache hujadili idadi ya wapiganaji, kikosi hicho kwa sasa kimeogezeka na kuwa na zaidi ya wanajeshi 7,000, wakigawika katika makundi kadhaa - vikosi vitano vya askari wa miguu, vinne vya mizinga na kikosi cha vifaru.



No comments