WALIOPORWA FEDHA ZA MADUKA YA KUBADILISHIA PESA WAMERUDISHIWA

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema wafanyabiashara walioporwa fedha zao wakati wa nyuma, wamerejeshewa pesa zao na hivyo kuwarudishia furaha.

Alitoa kauli hiyo wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Clouds, akisema uongozi wa miaka miwili ya Rais Samia, umerudisha tabasamu na furaha kwa wengi waliopata taabu katika uongozi uliopita.

Alisema wanasiasa waliokimbia nchi wamerejea nyumbani kuendelea na siasa, wale wenye mahoteli ambao walizifunga kwa sababu ya enzi za ugonjwa wa Covid nao wamepewa kitu ili kuwarudisha kwenye uhai wa biashara zao.

No comments