MO HATIMAYE AMZUNGUMZIA HAJI MANARA

Rais wa heshima wa Simba SC Mohammed Dewji ‘MO’ amezungumzia mahusiano yake na aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara na kudai kuwa Manara amekuwa akimtukana na anaendelea kumtukana lakini yeye hana kinyongo naye na kubainisha kuwa amemsamehe na kwamba amemwachia Mungu.


“Turudi kwa huyu ndugu yetu, tumefanya naye kazi vizuri, najua kwamba alikuwa amenitukana na anaendelea kunitukana.”


“Lakini Mimi nimemsamehe, kwanini maisha ni mafupi, yamepita hata kama akiendelea kunitukana Mimi namsamehe na sio yeye kuna wengine pia ambao wamenisema vibaya na kunitukana.”


“Mimi ni aina ya mtu ambaye siweki chuki ndani ya moyo wangu. Mungu amenijalia vitu viwili, kwanza sina wivu na mtu, pili sibaki na kinyongo, manake ikitokea jambo Mimi nasamehe, namuachia mwenyezi” amesema MO.

No comments