SPIKA WA BUNGE GHANA AMPINGA RAIS AKUFO HADHARANI

 

Spika wa Bunge la Ghana, Alban Bagbin amempinga Rais Akufo Addo hadharani juu ya uwepo wa mapenzi ya jinsia moja katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo kufuatia kauli ya Rais Nakufo kuhusiana na suala hilo wakati akizungumza na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris aliyeitembelea nchi hiyo wiki hii.

Kumekuwa na vuguvugu kubwa kuhusiana na suala la mapenzi ya jinsia moja katika nchi za Afrika hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote. 

Spika huyo wa Bunge alisema chombo anachokiongoza kitatunga na kupitisha muswada utakaotoa adhabu kali kwa wale wote watakaobainika kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga.

Alimtaka Rais Addo kutokuingilia mchakato wa utungwaji muswada huo kwani hana mamlaka hayo. Spika huyo amesema majibu aliyotoa Rais Akufo mbele ya Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris sio majibu rasmi kwani serikali haina mamlaka ya kutunga sheria bali inao wajibu wa kutelekeza sheria zinazotungwa na Bunge.

 

No comments