MUNGU NI MUWEZA WA YOTE, ALIYEGONGWA NA MWENDOKASI AREJEA MTAANI

 


Maisha hayatabiriki. Mtu aliyegongwa na basi la Mwendokasi jijini Dar es Salaam mwezi jana ambaye anafahamika kama Osam, hatimaye amerejea uraiani baada ya afya yake kutengemaa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa, Moi.

Ajali hiyo ambayo ilirekodiwa katika kamera za CCTV, ilikuwa mbaya kiasi kwamba ni watu wachache wanaweza kuamini kama mtu huyo, siyo tu alinusurika katika ajali hiyo, bali hivi sasa ni mzima anayeendelea na maisha mitaani.

No comments