SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA BARABARA YA NATA – SANZATE

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Vicent Mashinji, akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi. Eng. Godfrey Kasekenya, wakati akikagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Sanzate – Nata (km 40), kwa kiwango cha lami, mkoani Mara.

Serikali imewahakikishia wananchi wa Isenye, Wilaya ya Serengeti kuzimaliza changamoto zinazoukabili mradi wa ujenzi wa barabara ya Nata - Sanzate (km 40) kwa kiwango cha lami ili iweze kukamilika na kuondoa adha ya usafiri wanayoipata wananchi hao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akijibu maswali ya wananchi na kuahidi kutoa ushirikano kwa mkandarasi kwa kuonesha maeneo yote yenye changamoto ili yaweze kutatuliwa kwa haraka pindi ujenzi wa barabara hiyo unapoendelea.

Muonekano wa sehemu ya barabara ya Sanzate – Nata (km 40), inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mara.

Wananchi hao wameeleza changamoto hizo kuwa ni pamoja na kusuasua kwa mradi na mkandarasi kutoweka mifereji ya kupitisha maji na hivyo kuathiri makazi ya watu.


Naibu Waziri wa Ujenzi. Eng. Godfrey Kasekenya, akikagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Sanzate – Nata (km 40), kwa kiwango cha lami, mkoani Mara

"Siku zote unapohitaji maendeleo lazima kutakuwa na mabadiliko mengi ya utaratibu wa maisha yaliyokuwepo, na uwepo wa ujenzi wa barabara hii si kukomoa au kuonea watu bali ni kuleta manufaa makubwa na endelevu kwa jamii”, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya

 

No comments