PROF. MBARAWA: NI WAJIBU WA VIONGOZI KUBAINI MAPUNGUFU YA WATUMISHI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi  Profesa Makame Mbarawa amewataka viongozi wa  Sekta ya Uchukuzi, Idara na Taasisi zake kubaini mapungufu ya watumishi  na kuyafanyia kazi sanjari na  kuchukua   hatua za kinidhamu kwa watumishi wasio timiza wajibu wao.

 Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa   Baraza la wafanyakazi wa sekta ya Uchukuzi Profesa Mbarawa Amesema viongozi wa idara na taasisi ni wajibu wao kugundua changamoto za watumishi wa sekta na kuwachulia hatua wale wasio timiza wajibu wao. 


"Niwaombe viongozi wote wa  sekta ya Uchukuzi na Taasisi zake viongozi wabaini mapungufu yaliyopo kwa watumishi na kufanyia kazi  Aidha tusisite kuchukua hatua kwa watumishi wasio timiza wajibu wao.

Aidha ametoa rai kwa taaisisi zote zilizopo chini ya sekta ya uchukuzi kuhakikisha zinawashirikisha watumishi wao katika kupitia mipango na bajeti za taasisi kabla ya kuziwasilisha kwa msajili wa hazina.


 Kwa hatua nyingine Mbarawa amezitaka taasisi kuwasilisha michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kupunguza usumbufu kwa wastaafu ili kuepuka adhabu za tozo inayotokana na ucheleweshaji wa kuwasilisha michango hiyo.


"taasisi nyingi za Umma hazitekelezi wajibu huo na kuichafua serikali, hivyo kila taasisi ifanye uhakiki na uchambuzi wa madeni ya watumishi hususan wastaafu na kuainisha mikakati ya kulipa madeni 

No comments