RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKASIRIKA, AFOKA

 

Rais Samia Suluhu Hassan, kwa mara ya kwanza leo ameonyesha kukerwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali katika ubadhilifu wa fedha za umma.

Katika kikao kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali kwenye hafla fupi ya kupokea Taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2021/2022, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo, raia huyo namba moja alilazimika kutumia maneno makali kuonyesha kukerwa kwake.

Alisema kumekuwepo na tabia ya maofisa wa serikali kuongeza fedha katika malipo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali, wakati bei zilizoandikwa kwenye mikataba zikianisha wazi.


Alitolea mfano wa mradi wa ununuzi wa ndege inayotarajiwa kukamilika kutengenezwa na kuja nchini Mei, bei yake iliyo katika mkataba ni dola milioni 36, lakini jambo la kushangaza ni kwamba ankara ya malipo iliyowakilishwa serikali inaonyesha dola milioni 86, kitu ambacho kilimshangaza.

“Watu wa namna hii hawatakiwi kuwepo ofisini. Mtu anakuja na invoice kama hiyo, halafu unashindwa kumuuliza inakuaje, unamsikiliza anakuambia vifaa vimepanda bei, humuulizi mkataba unasemaje?”

No comments