MASHABIKI KUINGIA BURE BENJAMIN MKAPA LEO KUISHANGILIA TAIFA STARS
Wakati Taifa Stars ikijiwinda kupata ushindi mwingine dhidi ya The Cranes, mashabiki wameruhusiwa kuingia bure ili kutoa hamasa kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ikimenyana na Uganda leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Inafahamika kuwa shabiki namba moja wa Taifa Stars, Madam President Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi kadhaa kwa ajili ya mashabiki, kabla ya wadau wengine kujitokeza kumuunga mkono na kuwezesha uwanja mzima kujaa.
Rais pia atatoa shilingi milioni kumi kwa kila bao litakalopachikwa kimiani leo, sambamba na milioni 500 endapo watafuzu kwa Afcon 2024 kule Ivory Coast.

Post a Comment