CRDB, SILENT OCEAN WAINGIA MKATABA KUSAIDIA WAFANYABIASHARA
Benki ya CRDB na Kampuni ya Usafirishaji Mizigo ya Silent Ocean zimeingia makubaliano Machi 21, 2023 Jijini Dar es Salaam
ya kuwawezesha Wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi
kupitia kampuni hiyo waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka
gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini.
Hafla hiyo ya makubaliano imefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (kushoto) kwa Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo ya Silent Ocean, Salah Mohammed wakisaini hati ya makubaliano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni hiyo waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika Machi, 21 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.



Post a Comment