WAZIRI MKUU AWATAKA WAKUU WA MIKOA, POLISI KUWAKAMATA WAZAZI WALAWITI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Maofisa Ustawi wa Jamii wa mikoa yote nchini kuhakikisha inawasaka na kuwakamata mara moja wazazi na walezi wote wanaodaiwa kuwalawiti watoto wao.
Akiwa amekasirishwa na taarifa za kuwepo kwa mzazi anayedaiwa kumlawiti mwanaye mwenye umri wa miaka saba jijini Arusha, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa huo, John Mongela kuhakikisha mzazi huyo anatiwa nguvuni mara moja.
"Hizi taarifa za wazazi na walezi kuwalawiti watoto wao zinazidi kusikika kila siku, nawaagiza wakuu wa mikoa, makamanda wa polisi wa mikoa na maafisa ustawi, hakikisheni hawa watu wanakamatwa mara moja na kufikishwa katika vyombo vya sheria," alisema.
Vitendo hivyo vinavyozidi kushika kasi pamoja na mambo mengine, vinachangiwa na imani za kishirikina, upungufu wa afya ya akili na hata kukomoana miongoni mwa wazazi na walezi.

Post a Comment