WANAWAKE 66 WABAKWA, WAUME ZAO WAUAWA

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani la Amnesty International,limeripoti kuwa wanawake 66 walibakwa na waume zao kuuawa, vitendo vilivyofanywa na Waasi wa M23, wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.

Amnesty International wamesema bàada ya M23 kuudhibiti mji wa Kishishe, ulio km 100 Kaskazini mwa Goma, ambao ni mji mkuu wa Jimbo la Kivu, waasi hao waliingia nyumba kwa nyumba, ambako waliwaua wanaume wote waliowakuta na kuwabaka wanawake hao, wakati mwingine kwa makundi.

No comments