MCHUNGAJI ALIYESIMAMISHWA NA KUZUA TAHARUKI KKKT ASAMEHEWA BILA KOSA LAKE KUELEZWA
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Alex Malasusa ametangaza kumsamehe Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Usharika wa Kijitonyama, Eliona Kimaro.
Katika ibada iliyofanyika leo kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Malasusa aliwaambia waumini kuwa baada ya mchungaji huyo kuomba msamaha, kwa niaba ya kanisa, wameamua kumsamehe.
Januari 16 mwaka huu, Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, ilitangaza kumpa likizo ya miezi miwili mchungaji huyo bila kueleza sababu ya kufanya hivyo, kitu kikichosababisha taharuki kwa waumini waliotaka kutenguliwa kwa likizo hiyo.
Licha ya kupewa likizo hiyo, Kanisa pia lilimtaka Mchungaji Kimaro baada ya muda huo, kuripoti Makao Makuu ya Kanisa hilo.
Hata hivyo, pamoja na kumsamehe, halijaweza kuweka wazi kosa lililopelekea kupewa likizo yenye utata.

Post a Comment