FIKIRIA COLLABO YA WAKONGWE LADY JAYDEE, STARA, PROFESA JAY, SUGU, AFANDE SELE, SOLO THANG NA FEROOZ
Nimejaribu tu kufikiri kwa sauti.
Hawa ni wasanii bora kabisa wa muda wote wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama Bongo Fleva.
Wameukuza huu muziki hadi sasa vijana wanaogelea katika utajiri, lakini wanaimba mapenzi tu.
Hawa jamaa wanajua kutunga nyimbo zinazoakisi maisha na ukitaka ushahidi, sikiliza ngoma zao ambazo sasa zinaonekana za kizamani.
Walitumia muda mwingi kufikiri jamiii inachohitaji, wakapambana kuona lengo linafikiwa, lakini maisha yao kwa sasa hayabebwi na muziki.
Kama wangeamua kuingia studio na kutengeneza albamu, halafu wakaizindua pale Diamond Jubilee, ingekuwaje?

Post a Comment