AUAWA BAADA YA TREKTA ALILOKODI KUGONGA MTI WENYE MZINGA WA NYUKI
Mama mmoja kutoka Kijiji cha Miyale Karadoro, Wilaya ya Ugenya nchini Uganda, ameuawa baada ya trekta alilokodi kumlimia shamba lake kugonga kwa bahati mbaya mti aliokuwa amepumzika chini yake na mzinga wa nyuki uliokuwa juu kumwangukia.
Baada ya mzinga huo kumwangukia, nyuki hao walimshambulia kwa nguvu kiasi kwamba alishindwa kikimbia, hadi pale watu waliposogea na kutoa msaada akiwa hoi.
Jamaa hao walimpeleka hospitalini kwa matibabu lakini muda mchache baadaye alifariki dunia.
Imeelezwa kuwa familia ya mama huyo, imepata msiba wa pili ndani ya wiki mbili kwani siku chache zilizopita.
, mmoja wa wanafamilia alifariki nchini Marekani baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Post a Comment