DK HUSSEIN MWINYI AMKUMBUKA JPM CHAKECHAKE

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama kumkumbuka Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dokta Hussein Ally Mwinyi,leo amefanya ziara ya kushtukiza kwa wafanyabiashara wa vyakula huko Chake Chake Pemba.



Katika ziara hiyo, Rais Mwinyi alikagua bei ya bidhaa mbalimbali za vyakula na upatikanaji wake, sambamba na kuzungumza na wana chi.



Wakati wa uongozi wake, Dk Hussein akiwa Waziri wake wa Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JPM alijitengenezea sifa ya ziara zake za kushtukiza, ambazo nyingi ziliandamana na tumbuatumbua ya viongozi wa taasisi mbalimbali za umma.

No comments