KATIBU CCM WILAYA AONGOZA USAFI ENEO LA UJENZI OFISI MPYA
Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga, Mary Mwenisongole amewaongoza viongozi mbalimbali wa chama wilayani hapa kufanya usafi katika eneo ambako kutajengwa ofisi mpya, ambalo lipo mkabala ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya mjini hapa.
Katika zoezi hilo, viongozi wa matawi, kata, sekretarieti na jumuia za chama walishiriki.
Baadhi ya viongozi waliondamana na Katibu huyo ni pamoja Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya, Hajira Kapinga, Katibu wa Siasa na Uenezi John Bosco Mkandawile, Mwenyekiti UVCCM, Herswida Komba na Grace Mlinga ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake (UWT) wilaya.
Pia Mjumbe wa Kamati ya Siasa Gervas Nchimbi pia alishiriki zoezi hilo sambamba na madiwani wote wa Kata za Mbinga Mji.

Post a Comment