HATIMAYE MWILI WA MWANASOKA WA GHANA CHRISTIAN ATSU WAPATIKANA UTURUKI
Hatimaye, mwili wa mwanasoka wa kimataifa wa Ghana, Christian Atsu ambaye alifukiwa na vifusi kufuatia tetemeko la ardhi katika nchi za Uturuki na Syria, umepatikana.
Taarifa kutoka Uturuki zinasema mwili wa Atsu mwenye umri wa miaka 31,umepatikana wiki moja baada ya tetemeko hilo kubwa kutokea, ambalo hadi leo, limethibitisha vifo vya watu 45,000.
Wakala wa mchezaji huyo,Muret Uzunmehmet amethibitisha kifo cha mchezaji huyo ambaye alikuwa akichezea timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki ya Hatayspor.

Post a Comment