AFIKISHA UMRI WA MIAKA 97 MBINGA, AFANYIWA IBADA NYUMBANI KWAKE

Mzee Anton Daniel Matanila, leo ametimiza umri wa miaka 97, tangu alipozaliwa kijiji cha Mkumbi, kilometa 12 toka mjini Mbinga.

Ibada ya kumsalia mzee huyo ambaye katika maisha yake ameishi na wanawake wanne, akijaaliwa kupata watoto 27, wajukuu 51 na vilembwe 33, iliongozwa na Padre Beda kutoka Parokia ya Mtakatifu Kilian.

Ibada hiyo ikiyohudhuriwa na viongozi wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, Wanafamilia, ndugu, jamaa na majirani, ilifanyika nyumbani kwake eneo la Matarawe.



Father Beda, wakati akiongoza ibada hiyo, alisema amekuwa akija nyumbani hapo mara kwa mara kwa ajili ya kumpatia huduma ya kiroho na hivyo kupata nafasi ya kuzungumza naye.

Alisema kitu alichokigundua kutoka kwa mzee huyo ni kwamba mojawapo ya vitu vilivyomfanya aishi miaka mingi, ni roho yake ya kusamehe.



Mmoja wa dada wa Mzee Matanila, Rustika Kapinga akishangilia wakati wa sherehe hizo zilizoandaliwa na watoto pamoja na wajukuu.


MC wa shughuli hiyo, Moses Ndimbo 'Masinga' kulia,akimsikiliza mmoja wa wajukuu wa mzee Matanila, Rebecca Kapinga.


Diwani wa zamani wa Kata ya Mkumbi, Tomas Kapinga (kushoto), akiwa amekaa na Mzee Matanila wakati wa sherehe hiyo. Diwani huyo ni mwanafamilia ya mzee Matanila.



Mzee Matanila akimbusu mke wake mdogo aliye hai, Yusta Mbungu wakati wa sherehe hiyo.




Mzee Matanila akiinuliwa ili kwenda kukata keki ya kuadhimisha miaka 97 ya uwepo wake duniani.


Sehemu ya wanafamilia waliohudhuria hafla hiyo asubuhi ya leo hapa mjini Mbinga.


Misosi time. Wahudhuriaji wakipatiwa huduma ya chakula kuadhimisha miaka 97 ya maisha ya Mzee Matanila ambaye bado ana nguvu.

Mmoja wa watoto wake alisema mzee huyo bado ana kumbukumbu za kutosha kichwani mwake na kuwa amekuwa akijisaidia .wenyewe kwa mambo mengi isipokuwa mwendo mrefu.






No comments