KAJULA ABEBA MIKOBA YA GONZALES MSIMBAZI

Imani Kajula, ambaye anafahamika kuwa shabiki na mwanachama wa Klabu ya soka ya Simba ya Dar es Salaam, ametangazwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa miamba hiyo ya Kariakoo, akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Barbara Gonzales.

Barbara alijiuzulu nafasi ya CEO mwishoni mwa mwaka jana, katika uamuzi uliowashtua wengi, kwani mwanamama huyo alifahamika kwa uchapaji wake wa kazi.

Kajula, muajiriwa wa zamani wa Benki ya Posta na CRDB, amechukua mikoba hiyo kwa mkataba wa miezi sita.

No comments