MTOTO WA MIAKA SITA AJIUA KWA BASTOLA
MTOTO mwenye umri wa miaka 6, Erick
Mkandi ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Izumangambo
Mkoani Geita, amefariki dunia wakati akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali
ya Bwanga baada ya kujipiga risasi kwenye paji la uso na ikatokea kisogoni
akiwa ndani ya chumba cha Baba yake.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limesema tukio hilo limetokea
November 13,2021 katika Kitongoji cha Mkapa Kijiji cha Izumangambo .
RPC wa Geita, Henry Mwaibambe amesema silaha aliyoitumia
Mtoto huyo kujipiga risasi ni aina ya pistol Berreta yenye namba TZS
AR74955/E.86808Y ambayo inamilikiwa kihalali na Baba yake Mzazi aitwaye Joshua
Faustine huku chanzo cha tukio kikiwa ni Mtoto kutokujua madhara yatokanayo na
utunzaji mbaya wa silaha hiyo.
"Niwaombe Wamilki wote wa silaha wawe makini katika
kutunza silaha zao kwani wanapokuwa wanakabidhiwa wanaelekezwa namna ya kutunza
silaha hizo, RPC Geita.

Post a Comment