BINTI ATOZWA FAINI YA MILIONI NANE KUMFUATA RONALDO UWANJANI

 Inaweza kuwa picha ya Watu 5, watu wanasimama na nje

 

SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini Ireland FAI limempiga faini ya Irish £2500 (Milioni 8.3) shabiki mtoto Addison Whelan (11) kwa kitendo chake cha kuvamia eneo la kuchezea (Pitch) wakati timu yao ilipovaana na Ureno katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

Kupitia kituo cha Redio cha FM104 Addison Whelan amesema "Nimepigwa faini kwa kosa la kuingia uwanjani, baba anaenda kulipa"

"Niliingia uwanjani na kumkimbilia Ronaldo, walinzi walikuwa wananifuata nyumba na wengine wakitokea pembeni yangu"

"Nikawa naita jina la Ronaldo, kwa bahati nzuri akanisikia na kunigeukia, akawaambia walinzi waniache"

"Nilipofika nikamwambia, mimi ni shabiki wako mkubwa, naomba jezi yako, akanipa"

Hivyo ndivyo ndoto ya mtoto wa kike ilivyotimia

 

No comments