ZACHARIA HANS POPE AFARIKI DUNIA USIKU WA JANA

MWANAMICHEZO, Mfanyabiashara na
Mjumbe wa Bodi ya Klabu ya Simba, Zacharia Hanspope amefariki dunia jana usiku.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali,
Hanspope amefariki kutokana na ugonjwa wa corona. Mwenyekiti wa Bodi ya Simba,
Mohammed Dewji Mo, aliandika hivi kwenye ukurasa wake wa Instagram.
"Moyo wangu una maumivu makali
sana. Bado ni vigumu kuamini na kukubali kuwa mjumbe wetu, kaka yetu, Zakaria
Hans Poppe hatunaye tena.
"Kaka yangu, nimefanya kazi na wewe kwa miaka mingi, na
kila siku uliweka maslahi ya Simba mbele. Kaka yangu ulikua na wema wa kipekee,
na ulikua wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba, hukuwa na
maslahi binafsi. Ulikua rafiki wa marafiki wa Simba, na ulikua tofauti na
wasioitakia mema Simba.
"Kaka yangu, Umetangulia nasi tutafuata. Nitakukumbuka
sana kaka yangu. Natoa pole sana kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja
na wanafamilia wote na mashabiki wa Simba kwa kumpoteza ndugu yetu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi."

Post a Comment