JUMA UBAO AFARIKI DUNIA

MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi ambaye pia ni mwenyekiti
wa chama cha muziki wa Dansi (CHAMUDATA) Juma Ubao amefariki dunia leo asubuhi.
Juma Ubao aliyejulikana pia kama King Makusa, enzi za uhai wake
alitamba zaidi na bendi Biashara Jazz "Dunda Dunda".
Aidha, Juma Ubao ambaye alikuwa mwimbaji na mcharaza gitaa
mahiri, alitamba pia na kundi la 'zing zong' lililojulikana kama The Six
Manyara kwa kushirikiana na Hassan Rehan Bitchuka.
Taarifa za msiba wa Juma Ubao zimetolewa na Katibu wa CHAMUDATA
Hassan Msumari.
Said Mdoe 11/9/2021

Post a Comment