WAZIRI MKUU KUHOJIWA KWA MAUAJI YA RAIS

 Haiti: Ariel Henry assumes post as prime minister | News | DW | 20.07.2021


MWENDESHA Mashtaka Mkuu Nchini Haiti amemtaka Waziri Mkuu, Ariel Henry kueleza sababu za kuzungumza kwa simu na mmoja wa washukiwa wa mauaji ya Rais Jovenel Moise usiku wa tukio (Julai 7)

Barua iliyoandikwa kwa maneno ya hadhari inasema Henry alizungumza mara kadhaa kwa simu na mshukiwa mkuu, Joseph Felix Badio ambaye bado anatafutwa, alipokuwa karibu na eneo la mauaji.

Barua hiyo iliyotumwa Septemba 10, 2021 inasema "ingawa ni rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuamuru kuitwa kwenye mahojiano kwa mtu mwenye cheo chako, lakini kwa sasa Haiti haina Rais, nami nakualika kuhudhuria na kutoa ushirikiano."

No comments