YANGA YATEUA VIGOGO KUUNDA KAMATI YA MASHINDANO

 Mashabiki wampa heshima Injinia Hersi Said

IKIWA ni siku chache tu kabla ya kuanza kwa mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, mabingwa wa kihistoria nchini, Yanga, imeteua Kamati ya Mashindano inayowahusisha vigogo kadhaa wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya timu hiyo, Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla amewateua vigogo nane, ambao watakuwa chini ya Mwenyekiti, Rodgers Gumbo.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni pamoja na Davis Mosha, Seif Magari, Abdalahg Bin Kleb, Hamad Islam, Injinia Hersi Said, Lucas Mashauri, Arafat Haji na Peregrinius Rutayunga.

No comments