WIZARA YA UJENZI NA JWTZ ZAAHIDI KUKUZA USHIRIKIANO

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, ameliombaJeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara yake   katika   utekelezaji   wa   miradi   mbalimbali   inayosimamiwa   na  Wizara hiyo nchini.

Akizungumza   katika   kikao   cha   kufahamiana   na   kubadilishana   uzoefu   na Mnadhimu   Mkuu   wa   Jeshi   la   Wananchi   Tanzania   (JWTZ), Luteni Jenerali  Methew Edward Mkingile, Dkt. Chamuriho, amesema kuwa licha ya Wizara kutumia wataalam mbalimbali katika miradi ya Ujenzi, bado inahitaji ushirikiano na  wataalam kutoka katika Jeshi hilo.

“Nakupongeza kwa uteuzi uliopata, naamini kuwa uteuzi huu utakuwa chachu ya kuendeleza   ushirikiano   tuliokuwa   nao   na   kusaidia   katika   mwendelezo   wa utekelezaji   wa   miradi   inayosimamiwa   na   Wizara”,   amesema   Waziri   Dkt.Chamuriho.

Aidha,   Dkt.   Chamuriho   amesisitiza   kuwa   kutumia   wataalam   shirikishi   kutoka katika   Jeshi   hilo   imekuwa   ni   msaada   mkubwa   katika   kuhakikisha   miradi inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha na kukamilika kwa wakati. Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Methew Edward Mkingile, ameipongeza Wizara hiyo kwa kutoaushirikiano wa kutosha kwa Jeshi hilo na kuwaamini katika kutekeleza miradi yaWizara.

“Sisi tupo tayari na bado tutaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara na Taasisi za Serikali kama Sheria inavyotutaka, lengo ni kuhakikisha malengo na maendeleo ya nchi yanafikiwa”, amesisitiza Luteni Jenerali Mkingile.

Uongozi   wa   Wizara   umekutana   na   Mnadhimu   Mkuu   wa   Jeshi   la   Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Methew Edward Mkingile, ikiwa ni siku kadhaa mara baada ya uteuzi wake ambapo pamoja na mambo mengine ziara hii ilikuwa na lengo la kuendeleza na kukuza ushirikiano baina ya Taasisi hizo.

 Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

No comments